Showing posts with label matukio. Show all posts
Showing posts with label matukio. Show all posts

ANGEL DI MARIA AELEZA YALIO MSIBU MPAKA KUONDOKA MADRID SOMA UJUE SABABU

KISIWA CHA BURUDANI | 12:19 AM | 0 comments

MAJONZI: BARUA YA ANGEL DI MARIA YAWALIZA REAL MADRID..SOMA ZAIDI HAPA!

Written By Jo Cyberspace on Wednesday, 27 August 2014 | 22:14

Kiungo mshambuliaji mpya wa Manchester United, Angel Di Maria ameandika barua iliyowasikitisha wachezaji na mashabiki wa Real Madrid.

Di Maria ambaye ametua Man United kwa dau la pauni milioni 60 ambalo ni rekodi England, amesema hakupanga kuiacha timu hiyo ya Hispania. 
Mashabiki waliochangia kwenye mtandao wa Twitter wameelezwa kusikitishwa na barua hiyo huku wakiamini siku moja, Di Maria atarejea tena katika klabu yao. 

Amesema wakati anakwenda kwenye Kombe la dunia baada ya kutwaa ubingwa wa Ulaya ‘La Decima’ akiwa na Madrid, alitarajia kurudi na kuendelea na kazi yake.
“Hata hivyo kuna mambo yalijitokeza, yakiwemo ya mshahara wangu na sasa natarajia kuyapata Manchester United, moja ya klabu kubwa duniani na nina imani nitaweka historia pale,” alieleza katika sehemu ya barua hiyo.


Di Maria ameeleza atakavyowakumbuka wachezaji wengi wa Madrid na maisha yao kwa ujumla.Tayari Muargentina huyo amemalizana na Man United na baadhi ya wachezaji wa Madrid kama Cristiano Ronaldo na Sergio Ramos, hawakutaka aondoke.

https://wwwVIDEO YA NYOKA MKUBWA NA HATARI SANA ...... .youtube.com/watch?v=yfdCiwzhNN0&list=PLu03VTrb5fmYRtsv8leFHpMmrDWiVScv1&feature=player_embedded

KISIWA CHA BURUDANI | 10:04 PM | 0 comments
https://www.youtube.com/watch?v=yfdCiwzhNN0&list=PLu03VTrb5fmYRtsv8leFHpMmrDWiVScv1&feature=player_embedded
diving-huge-snake

HUYU NDIE NYOKA MKUBWA KULIKO WOTE JIONEE PICHAZAKE..............................

KISIWA CHA BURUDANI | 9:56 PM | 0 comments
diving-huge-snake  

massive-20-foot-snakegreen-anaconda-river
Franco-Banfi-Giant-Anaconda-Divercaught-camera-snake

MNYAMA WA WAJABU MUKILISHA AMANI ATOKEA TANZANIA......

KISIWA CHA BURUDANI | 10:30 PM | 0 comments
WAKAZI wa eneo la Sensera Pub, Mbezi Juu jijini Dar es Salaam wamefurika kumuona mnyama aina ya kakakuona ambaye alijitokeza juzi usiku.


Taarifa za kujitokeza kwa mnyama huyo zilisambaa hadi chumba cha habari cha gazeti hili ambalo lilifika eneo hilo na kushuhudia umati wa watu ukiwa nje ya nyumba ya Martha Boniface ambaye alikuwa amemfungia kwenye moja ya vyumba vyake vya biashara.


Martha ambaye alikuwa mtu wa kwanza kumuona mnyama huyo ambaye ni aghalabu kuonekana, akitumika kama mtabiri wa mambo makubwa yanayoweza kutokea katika taifa, alisema alikiona kiumbe hicho juzi saa tano usiku kikiwa kinapita kwa mwendo wa taratibu.


“Tulikuwa tumekaa na wenzangu kama watano hapa nje jana (juzi) usiku, mara mmoja wetu akasimama akasema jamani mdudu huyo, niliponyanyuka nikamuona kakakuona anatembea anakuja tulipokaa, tulimpisha akasimama, badae akajikunja, tukamnyanyua na kumuingiza kwenye boksi kumuhifadhi,” alisema Martha.


Alisema baada ya kumuingiza kwenye boksi, walimpeleka ndani ya chumba cha ‘stationary’ na baadae ndani ya boksi ili aweze kuzunguka.
“Usiku ule ule nilichukua maji, kisu, unga na fedha shilingi 10,000 nikamuwekea vyote kwa pamoja, maji alikunywa yote, na unga alikula wote, fedha aliisogelea akainusa, lakini kisu alikipita akakiruka, hakukigusa wala kukinusa,” alisema Martha.


Akielezea sababu ya kumfungia ndani ya chumba hicho, Martha alisema alilazimika kuchukua hatua hiyo ili asiondoke.


“Na usiku ule ule kabla sijafunga nikamtandikia kiroba ili asipate baridi la sakafu, lakini asubuhi nilimkuta kalala chini,” alisema Martha.


Kulingana na imani zilizopo nchini, kitendo cha mnyama huyo kula na kugusa vitu hivyo vitatu kati ya vinne, baadhi wanatafsiri kuwa ni ishara ya nchi kuwa na amani, mavuno mazuri na mvua za kutosha.


Kwa upande wake, Martha anachukulia kitendo cha kumuona kakakuona kinatoa tafsiri ya neema na bahati ambayo ameshushiwa na Mungu kwani kiumbe huyo huonekana mara chache.


MTANZANIA Jumapili lilishuhudia baadhi ya wananchi waliofika katika eneo hilo kwa nia ya kukishuhudia kiumbe hicho wakishikwa na mshangao wakati Martha akijaribu kukibembeleza kijikunjue katika gamba lake analolitumia kujificha ili kiweze kuonekana vizuri.


“Mgeni naomba uamke uwasalimie wenyeji wako wamekuja kukuona, tunajua umekuja kwa nia nzuri, umetuletea baraka, lakini watu wanatamani kukuona, naomba ujifungue ili uwasalimie wenyeji wako,” alisikika akisema Martha wakati akijitahidi kukifanya kiumbe hicho kijikunjue.


Baada ya muda kakakuona alianza kufungua miguu yake yote na kisha mkia, na baadae akaanza kutembea akizunguka huku na huko ndani ya chumba hicho.


Aidha mmoja wa jirani wa eneo hilo, Syntyche Sanya, alisema kwa mara ya kwanza alimuona kakakuona katika eneo hilo Jumatano asubuhi wakati anaenda kazini.


“Mimi nilimuona saa 11 alfajiri wakati naenda kazini, kwa sababu nilikuwa simjui sikumfuatilia kabisa, nikajua ni mnyama wa kawaida,” alisema Sanya.
Mume wa Martha, Boniface Machera, alisema amefurahishwa na ujio wa myama huo mtaani kwao, lakini kutokana na umuhimu wake, waliamua kumuhifadhi hadi watendaji kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii watakapokuja.


“Tumemuhifadhi kwa sababu akiondoka kuna mawili, anaweza akapotea au watu wakamkamata na kumtoa magamba,” alisema Machera.
Aidha baadhi ya vijana waliofika kumuona kakakuona, walitumia tukio hilo kufanya utani.


Mmoja wa vijana hao alisikika akisema: “Tumemuwekea bendera mbili, ya CCM na Chadema, lakini akaenda kuegemea ya Chadema,” alisema huku wenzake wakiangua kicheko.


Hata hivyo, alipoulizwa Boniface kuhusu taarifa hizo, alicheka na kusema kuwa walikuwa wanatania tu na hakuna bendera yoyote iliyowekwa.

Mara ya mwisho mnyama huyo alionekana jijini Dar es Salaam Julai mwaka jana katika eneo la Buza na mwaka huu ni mara ya kwanza kujitokeza.


Alionekana pia Oktoba mwaka 2010 katika eneo la Bunju ambako wananchi walimuwekea nafaka, silaha za jadi, maji na vitu vingine, lakini alienda kuegemea panga akiashiria hatari.

SAMAKI MWENYE UREFU WA FUTI 3 AVULIWA KIRAHISI................

KISIWA CHA BURUDANI | 11:04 AM | 0 comments
Samaki aliye na urefu wa mita tatu aliyekuwa maarufu katika mto Amazon amevuliwa hadi ameangamia
Watafiti wamedhihirisha kuwa samaki huyo mkubwa hapatikani tena katika maeneo aliyokuwa maarufu.
Imebainika sasa kuwa samaki wa Arapaima alipatikana katika maeneo 8 kati ya 41 zilizofanyiwa utafiti, na idadi ya samaki huyo ilikuwa ndogo sana kulikoilivyokuwa inatarajiwa.
Wavuvi walipewa mafunzo jinsi ya kuhesabu samaki hao ili kufanikisha utafiti huo mkubwa.
Watafiti walikata kauli kuwa athari za uvuvi kwa samaki wa kitropiki zilikuwa mbaya zaidi ya ilivyoaminika hapo awali.
Matokeo ya utafitihuo yaliripotiwa kwa shirika la uhifadhi wa mazingira yanayozalisha viumbe vya majini ''Aquatic Conservation: Freshwater and Marine Ecosystems''.
Arapaima huweza kuwa na uzani wa kilo 181 na ni mojawapo ya samaki wakubwa zaidi wanoishi katika maji yasiyo na chumvi.
Samaki hao hupumua hewa sawa na binadamu, hivyo basi huibuka kutoka majini kupumua kila baada ya dakika kati ya 10-15 hivyo basi huwa ni rahisi kuwakamata.
Ukubwa wa Arapaima huvutia wavuvi kuwawinda na aghalabu huwanasa kwa kutumia chusa au nyavu za uvuvi.
Karne moja iliyopita, idadi ya Arapaima ilikuwa kubwa katika mto wa Amazon, lakini watafiti wanasema kuvua kupita kiasi kumesababisha idadi hiyo kupungua kwa kiwango kikubwa sana.
Hapo awali, utafiti nadharia ulitabiri kuwa uvuvi hauwezi kuangamiza aina fulani ya samaki majini kwani wavuvi huenda kuvua maeneo tofauti idadi ya samaki inapopungua katika eneo moja.
Wanasayansi, wakiongozwa na Leandro Castello, kutoka Virginia Marekani, walitaka kufahamu afya ya samaki wa Arapaima walioko eneo la chini la Amazon.
Aidha walitaka kugundua iwapo shughuli za uvuvi ziliunga mkono au kupinga utabiri wa nadharia tofauti.
Kuna nadharia zinazopendekeza kuwa samaki wakubwa, walio ghali, na ambao ni rahisi kukamatwa huweza kuvuliwa na kuisha majini, huku nadharia zingine zikipinga msimamo huo.
Watafiti hao walihoji wavuvi 182, walioaminika kuwa magwiji na wenzao, katika jamiii 81, zinazoishi katika eneo la kilomita 1,040, la Amazon.
Shughuli hiyo ilijumuishwa hesabu ya Kulifanywa ya samaki katika jamii 41 kati ya jamii zilizohojiwa.
Wavuvi nane walifunzwa kuhesabu idadi ya Arapaima pindi tu walipotokea majini.
Matokeo ya hesabu hiyo ni kuwa idadi ya Arapaima ilikuwa imepunguka katika asilimia 57% ya eneo la utafiti, Arapaima hawakuwepo katika asilimia 19% ya eneo hilo, na walivuliwa kupita kiasi katika asilimia 17% ya eneo hla utafiti, huku asilimia 5% tu wakifanya uvuvi unaokubalika.
Kwa 2% ya jamii zilizofanyiwa utafiti, samaki hao h

EBOLA NDANI YA TANZANIA

KISIWA CHA BURUDANI | 11:08 PM | 0 comments

Mhudumu wa afya akiwa katika hali ya tahadhari ya Ebola huko Afrika Magharibi
Kuna taarifa ya kuwepo kwa mtu mmoja anayehisiwa kuwa na virusi vya ugonjwa wa Ebola nchini Tanzania.
Kwa mujibu wa Mkuu wa Kitengo cha mawasiliano wa Wizara ya Afya ya Tanzania Nsachris Mwamaja mtu huyo ana asili ya Afrika Magharibi ambaye ni mkazi wa mji wa Dar es Salaam ambaye alifika katika hosptali moja akiwa na homa kali ikiwa ni dalili mojawapo ya ugojwa huo .
Bwana Mwamaja amesema mgonjwa huyo ambaye ni mtoto wa makamo tayari ameshatengwa na yupo chini ya uangalizi wa karibu madaktari katika hosptali Temeke ambayo ni ndio iliyotengwa kwa ajili ya watakaohisiwa kuwa na ugonjwa huo.
Amesema sababu nyingine ya kuhisiwa kwa mtu huyo kuwa huenda ameambukizwa virusi vya ugonjwa huo ni kwa vile hivi karibuni alitokea nchini Benin.
Hii ni mara ya kwanza ya kuwepo kwa taarifa za mtu kuhisiwa kuwa na virusi vya Ebola nchini Tanzania.
Taarifa hizi zinakuja baada ya hapo awali serikali ya nchi hiyo kukanusha taarifa iliyotolewa na gazeti moja la udaku kuwa kuna mgonjwa mmoja wa Ebola aliyegundulika nchini Tanzania.

Taarifa zinazohusiana

EPHRAHIM KIBONDE ALIVYODHALILISHWA NA TRAFIKI BAADA YA KUSABABISHA AJALI.

KISIWA CHA BURUDANI | 3:06 AM | 0 comments
Mtangazani Mahiri wa Redio Clouds FM Ephrahim Kibonde akidhibitiwa na Askari wa Usalama barabarani.
*****************
Kibonde anadaiwa kusababisha ajali  juzi asubuhi  eneo la Makumbusho, baada  ya gari aliyokuwa akiendesha kuigonga gari ya dereva mwingine kwa nyuma. Trafiki walifika eneo la tukio na kupima ajali, Kibonde alipoona hivyo akarudi nyuma na kuendesha gari lake kuondoka eneo la tukio bila kufuata taratibu za usalama barabarani,hali iliyomlazimu yule Trafiki kutumia gari lililogongwa kumfukuzia.

Walifanikiwa kumkamata eneo la Mwenge na Trafiki aliingia katika gari lake na kumwomba arudi eneo la ajali ili wakapime na kuchora mchoro wa ajali. Kibonde aligoma na kumtaka trafiki ashuke katika gari lake,Trafiki naye  aligoma kushuka na kumuamuru Kibonde arudi eneo la tukio.

Kibonde aliondoa gari na kuendelea na safari yake huku yule Trafiki akiwa ndani ya gari hiyo, Trafiki aliwasiliana na wenzake ambao walianza kuifuatilia gari hiyo ya Kibonde kama walivyopewa maelekezo na mwenzao aliyepo ndani ya Gari hiyo.

Mara Kibonde akatokea maeneo ya mataa ya Ubungo, hapo kulikuwa na Trafiki mwingine aliyekua eneo hilo akaipiga mkono gari ya Kibonde na ambapo inasemekekana hakusimama na badala yake ikaja gari nyingine na kuichomekea kwa mbele na hapo ndipo alipotiwa mbaroni!

Aligoma kuendesha gari ikabidi livutwe hadi polisi Urafiki na yeye kuwekwa chini ya ulinzi na baadae akahamishiwa Kituo cha Oystabay ambako yupo mpaka sasa.

Inadaiwa kuwa Kibonde alikuwa amelewa sana,hali iliyopelekea kufanya hayo yote ikiwa ni pamoja na kuwajibu vibaya Askari hao.

 
Copyright © 2011. KISIWA CHA BURUDANI - All Rights Reserved