Home » » EPHRAHIM KIBONDE ALIVYODHALILISHWA NA TRAFIKI BAADA YA KUSABABISHA AJALI.

EPHRAHIM KIBONDE ALIVYODHALILISHWA NA TRAFIKI BAADA YA KUSABABISHA AJALI.

KISIWA CHA BURUDANI | 3:06 AM | 0 comments
Mtangazani Mahiri wa Redio Clouds FM Ephrahim Kibonde akidhibitiwa na Askari wa Usalama barabarani.
*****************
Kibonde anadaiwa kusababisha ajali  juzi asubuhi  eneo la Makumbusho, baada  ya gari aliyokuwa akiendesha kuigonga gari ya dereva mwingine kwa nyuma. Trafiki walifika eneo la tukio na kupima ajali, Kibonde alipoona hivyo akarudi nyuma na kuendesha gari lake kuondoka eneo la tukio bila kufuata taratibu za usalama barabarani,hali iliyomlazimu yule Trafiki kutumia gari lililogongwa kumfukuzia.

Walifanikiwa kumkamata eneo la Mwenge na Trafiki aliingia katika gari lake na kumwomba arudi eneo la ajali ili wakapime na kuchora mchoro wa ajali. Kibonde aligoma na kumtaka trafiki ashuke katika gari lake,Trafiki naye  aligoma kushuka na kumuamuru Kibonde arudi eneo la tukio.

Kibonde aliondoa gari na kuendelea na safari yake huku yule Trafiki akiwa ndani ya gari hiyo, Trafiki aliwasiliana na wenzake ambao walianza kuifuatilia gari hiyo ya Kibonde kama walivyopewa maelekezo na mwenzao aliyepo ndani ya Gari hiyo.

Mara Kibonde akatokea maeneo ya mataa ya Ubungo, hapo kulikuwa na Trafiki mwingine aliyekua eneo hilo akaipiga mkono gari ya Kibonde na ambapo inasemekekana hakusimama na badala yake ikaja gari nyingine na kuichomekea kwa mbele na hapo ndipo alipotiwa mbaroni!

Aligoma kuendesha gari ikabidi livutwe hadi polisi Urafiki na yeye kuwekwa chini ya ulinzi na baadae akahamishiwa Kituo cha Oystabay ambako yupo mpaka sasa.

Inadaiwa kuwa Kibonde alikuwa amelewa sana,hali iliyopelekea kufanya hayo yote ikiwa ni pamoja na kuwajibu vibaya Askari hao.

Share this article :
 
Copyright © 2011. KISIWA CHA BURUDANI - All Rights Reserved