Home » » Prof. Lipumba: rais jk anauwezo wa kuvunja bunge............ila??? bofia more upate ukweli wa mambo

Prof. Lipumba: rais jk anauwezo wa kuvunja bunge............ila??? bofia more upate ukweli wa mambo

KISIWA CHA BURUDANI | 10:45 PM | 0 comments


Prof. Lipumba: Kikwete ana uwezo wa kuvunja Bunge la Katiba kwa mamlaka aliyo nayo

Posted By - (4418) Views

MWENYEKITI Mwenza wa Kundi la Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), Prof. Ibrahim Lipumba, amemtaka Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete, kutumia mamlaka aliyonayo kama Mkuu wa nchi kulivunja Bunge Maalum la Katiba linaloendelea na shughuli zake mjini Dodoma.
Prof. Lipumba amesema hayo leo Ijumaa Agosti 15, 2014 wakati akizungumza kwenye kipindi cha ‘Tuongee asubuhi’ kinachorushwa na Kituo cha runinga cha Star Tv.
Amebainisha kuwa kuendelea kwa vikao vya bunge hilo bila kuwepo kwa maridhiano baina ya makundi muhimu ni matumizi mabaya ya fedha za mlipa kodi na kuongeza kuwa hali hiyo itapelekea kupatikana kwa katiba ambayo haitakubaliwa na wananchi kutokana na msuguano unaoendelea kwa kutafuta katiba kwa ubavu wa kisiasa.
Aidha, amesema licha ya sheria ya kutomruhusu Rais kulivunja bunge hilo, bado anaamini kuwa Rais Kikwete, ana nia ya dhati ya kuunda Katiba bora na kwamba anaweza kutumia mamlaka yake kwa kuwa ni Mkuu wa nchi tofauti na inavyotafsiriwa na watu mbalimbali kwa ajili ya kuepuka kutumia gharama zisizo za lazima bila maridhiano.
Amelaani kitendo cha wajumbe kutoka kundi la walio wengi na wajumbe wa kundi la 201 kuendelea na vikao bila kuwepo na kundila UKAWA hakuwezi kuwapatia watanzania Katiba iliyobora.
Hata hivyo, hapo jana Agosti 14, 2014 Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu, ilieleza kuwa Rais Kikwete, hana mamlaka kisheria ya kulivunja bunge hiloambalo kwa sasa linamaliza takribani wiki mbili tangu lianze vikao vyake mjini mjini Dodoma Agosti 5, 2014.
Kumekuwepo na maombi mengi tangu UKAWA kususia vikao vya bunge hilo kutoka kwa taasisi na makundi tofauti yakimtaka Rais Kikwete kuvunja Bunge hilo kutokana na mwenendo wa kile kilichoitwa kuwa serikali inatumia mabavu katika kutengeneza Katiba kwa ajili ya Watanzania.
Share this article :
 
Copyright © 2011. KISIWA CHA BURUDANI - All Rights Reserved