Deni hilo linatokana na gharama za uchapishaji tiketi za kuingilia
uwanjani katika mechi za ligi kuu ya Tanzania tangu mwaka 1997.
TFF kwa sasa iko katika mpango wa kuuza tiketi
za uwanjani kwa njia ya ki-eletroniki (umeme) ikiwa ni sehemu ya
jitihada ya kupunguza adha kwa wapenzi wa soka na kudhibiti wizi na
ulanguzi wa tiketi.
Wambura amesema jitihada zinafanyika kumaliza
deni hilo, ila TFF italifuatilia kwa umakini na kuchunguza mwenendo
mzima uliosababisha kuwepo deni hilo.